rfi.myUNESCO: Watayarishaji wa maudhui wahimizwa kuhakiki taarifa kabla ya kuchapishaWatayarishaji wa maudhui ya mitandaoni wamehimizwa kuthibitisha taarifa kabla ya kuzisambaza, huku utafiti ukionyesha changamoto za upatikanaji wa mafunzo ya kuhakiki taarifa miongoni mwa watayarishaji hao wa kutoka mataifa mbalimbali.
RFI Kiswahili
RFI Kiswahili
@sw.rfi.fr
🌍 Idhaa ya kiswahili ya @RFI.fr (Radio France Internationale) ipo kwa kukuhabarisha habari za kimataifa 💻 rfi.fr/sw/ 🎧 rfi.my/mubashara 𝕏 rfi.my/Xsw 📷 rfi.my/IGsw 🗨️ rfi.my/WAsw
66 followers6 following7.3K posts
rfi.myMkuu wa usalama wa Iran akutana na kiongozi wa kiroho Mojtaba KhameneiMkuu wa usalama wa Iran Mohsen Rezaei, Jumanne ya wiki hii, alikutana na kiongozi wa juu wa kiroho nchini humo Ayatollah Mojtaba Khamenei, ambaye hajaonekana hadharani tangu kuuawa kwa babake yake mwezi Machi, mkutano wao ukifanyika ikiwa imepita siku moja tangu Tehran kushiriki mazungumzo na wawakilishi wa Saudi Arabia, Uturuki Pakistan.
rfi.myDRC: Upinzani unakataa mabadiliko yoyote ya katiba na matumizi ya nguvu kwa kuchukua madarakaaViongozi watano wa vyama vya upinzani vinavyounda muungano wa C64 wanaokutana mjini Roma kuanzia Oktoba 25 hadi 27, 2026, unapendekeza mikutano tofauti na Félix Tshisekedi na Joseph Kabila ili kutafuta suluhisho la mazungumzo kwa mgogoro wa Kongo. Tamko lao la mwisho linalaani jaribio lolote la kusalia madarakani nje ya mipaka ya katiba na kunyakua madaraka kupitia mtutu wa bunduki.
rfi.myAlexia Putellas wa Uhispania na Harry Kane wa Uingereza wametunukiwa taji la Ballon d'Or 2026Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Bayern Munich, Harry Kane, na nyota wa Uhispania, Alexia Putellas, wametangazwa rasmi kuwa washindi wa tuzo za Ballon d'Or 2026 kwenye sherehe ya kihistoria iliyofanyika jijini London. Huu ulikuwa usiku wa kipekee kwani kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo mwaka 1956, sherehe hizi zilifanyika nje ya nchi ya Ufaransa.
rfi.myKylian Mbappé azua hasira nchini China baada ya matamshi yake kuhusu Mao ZedongMchezaji nguli wa Real Madrid, raia wa Ufarasa, Kylian Mbappé anakabiliwa na kashfa kubwa nchini China na kusitishwa mara moja kwa mikataba kadhaa ya matangazo ya biashara baada ya kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii ambapo alionekana kufanyia mzaha picha (meme) inayomwonyesha akiwa amefananishwa na kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Mao Zedong, na kumwita "dikteta".
rfi.myBrazil: Jaji aagiza uchunguzi kuhusu uwezekano wa ufadhili wa kigeni kwa kampeni ya BolsonaroJaji wa Mahakama Kuu ya Brazil siku ya Jumanne, Oktoba 27, ameagiza uchunguzi ufanyike, kuhusu uwezekano wa ufadhili wa kigeni kwa kampeni ya mgombea wa kihafidhina Flavio Bolsonaro, ambaye alishindwa na Lula katika raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.
rfi.myNiger yalaani shambulio la ndege zisizo na rubani kutoka Chad kwa 'uungaji mkono wa Ufaransa'Niger imemwita balozi wa Chad kufuatia shambulio la ndege zisizo na rubani katika eneo lake. Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa siku ya Jumatatu, Oktoba 26, serikali ya Niger ililaani "shambulio la ndege zisizo na rubani lililofanywa kutoka eneo la Chad" ambapo, inadai, Ufaransa ilishiriki. Tukio hilo linakuja huku uhusiano kati ya Niamey na N'Djamena ukiendelea kuzorota.
rfi.myUmoja wa Mataifa: China yataka kutetea uwakilishi bora wa Afrika katika Baraza la UsalamaChina inataka kuzungumza kwa niaba ya nchi za Ukanda wa Kusini mwa Dunia (Global South), ikidai jukumu hilo kwa kushinikiza mageuzi ndani ya Umoja wa Mataifa (UN). Katika Jukwaa la Kimataifa la Utawala Bora mjini Xiong’an, Waziri wa Mambo ya Nje alisisitiza umuhimu wa uwakilishi mzuri zaidi wa Afrika katika Baraza la Usalama la UN.
rfi.myUrusi: Tume ya uchunguzi inaelezea 'usafirishaji haramu wa binadamu' wa wale waliotumwa Ukraine"Usafirishaji Haramu wa Binadamu": hivi ndivyo tume huru ya kimataifa ya uchunguzi kuhusu Ukraine inavyoelezea kuajiri wageni kwa lazima na jeshi la Urusi katika ripoti yake ya hivi karibuni iliyowasilishwa Oktoba 26 kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
rfi.myRDC: Mkutano wa viongozi watano wa C64 unaendelea nchini ItaliaMkutano wa viongozi watano wa vyama vya upinzani vinavyounda muungano wa C64 Jumanne hii unaingia katika siku yake ya pili mjini Roma, Italia ambapo viongozi hao Wanatarajiwa kuwasilisha hitimisho lao kwa waandishi wa habari baadaye asubuhi hiyo.
rfi.myCanada: Vijana 15 wameishtaki serikali kwa kutochukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchiMahakama ya Canada inasikiliza kesi iliyowasilishwa na vijana 15 dhidi ya serikali ya nchi hiyo siku ya Jumatatu, Oktoba 26, kwa kutochukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Vijana hao wanasema kwamba Canada haipunguzi vya kutosha uzalishaji wake wa gesi chafuzi na kwamba athari za mabadiliko ya tabianchi zinakiuka haki yao ya kikatiba ya kuishi.
rfi.myKuzuiliwa kwa Kaka: "Ikiwa mamlaka haijasema chochote, ni kwa sababu hajafanya uhalifu wowote"Mwanahabari mwenzetu Moussa Kaka, ambaye ulisikia akiripoti habari za nchi yake kwa miaka mingi kwenye RFI, hajasikika tangu jioni ya Agosti 31. Hatimaye, utawaa wa kijeshi nchini Niger umethibitisha kwamba anashikiliwa, lakini bila kutaja makosa anayoshukiwa. Wenzake wengi kote barani Afrka wanaendelea kuonyesha mshikamano wao, akiwemo Venance Konan, mkurugenzi wa zamani wa Gazeti la kila siku la Côte d'Ivoire, Fraternité Matin.
rfi.myMkutano wa Bioanuwai wa COP-17 unaingia katika wiki yake ya pili, chini ya vikwazo vikubwaMkutano kuhusu bioanuwai COP17 unaingia wiki yake ya pili huko Yerevan, Armenia. Wawakilishi kutoka karibu nchi 200 wanafanyia kazi jinsi ya kuimarisha hatua za kukomesha uharibifu wa asili unaosababishwa na shughuli za binadamu ifikapo mwaka 2030. Maendeleo yanafanywa, ingawa baadhi ya masuala yanabaki kuwa chini ya vikwazo vikubwa, hasa upande wa kifedha.
rfi.mySaudi Arabia, Uturuki, na Pakistan zakutana Tehran ili kuepuka vita vya kikandaJe, kuongezeka kwa mapigano kati ya Riyadh na Tehran kunaweza kuepukwa? Hili ndilo swali kuu la majadiliano yaliyopangwa kufanyika Jumatatu, Oktoba 26, katika mji mkuu wa Iran. Maafisa wakuu kutoka muungano wa kijeshi wa Mkataba wa Makka—ulioundwa na Saudi Arabia, Uturuki, na Pakistan—watakutana na viongozi wa Iran. Mkutano huo unatarajiwa kuwa na mvutano mkubwa, kwani Riyadh mara kwa mara hukabiliwa na mashambulizi kutoka kwa waasi wa Houthi, ambao wanaungwa mkono na Iran.
rfi.myAfrika Kusini: Tume ya AU yalaani mauaji ya raia wa kigeni jijini DurbanTume ya Afrika ya Haki za Binadamu inatoa wito kwa Afrika Kusini kutangaza mashambulizi dhidi ya wageni kuwa mgogoro, huku wimbi la chuki dhidi ya wageni ambalo limeikumba Afrika Kusini kwa miezi kadhaa na kuwafukuza makumi ya maelfu uhamishoni likiendelea bila kukoma. Taarifa kutoka kwa chombo cha Umoja wa Afrika inafuatia kifo cha raia wa kigeni katika mitaa ya Durban wiki iliyopita, aliyepigwa hadi kufa na waandamanaji zaidi ya hamsini wenye chuki dhidi ya wageni.
rfi.myRDC: Prince Epenge, msemaji wa Lamuka azuiwa kusafiri kwenda RomaNchini DRC, Prince Epenge, msemaji wa muungano wa kisiasa wa Lamuka, unaongozwa na Martin Fayulu, alikamatwa na maafiasa wa usalama na kupelekwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa N'djili, jijini Kinshasa na kupelekwa kusikojulikana, wakati akielekea jijini Roma, kwa ajili ya mkutano wa wapinzani.
rfi.myTanzania: Lissu anatarajiwa kuanza mgomo wa kula na kutumia dawaNchini Tanzania, kuelekea uamuzi wa kesi ya uhaini tarehe sita mwezi Novemba, inayomkabili, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tundu Lissu, anatarajiwa kuanza mgomo wa kula na kutumia dawa kwa kile anachosema idara ya Magereza nchini humo, imemnyima haki ya kukutana na Mawakili wakati huu anapoendelea kuzuiliwa.
rfi.myOrmiston anyakua dhahabu, Miro aota ubingwa wa dunia katika mashindano KisumuCallum Ormiston wa Afrika Kusini ametwaa ubingwa wa mbio za barabarani za wanaume wakubwa katika Mashindano ya Afrika ya Baiskeli za Barabarani ambayo yametamatika leo mjini Kisumu, huku Paul Miro wa Uganda akijinyakulia medali ya shaba katika kitengo cha wanaume wasiozidi umri wa miaka 23 na kuweka macho yake kwenye ubingwa wa dunia.
rfi.myKenya: Mzozo unaongezeka baada ya jengo kuanguka jijini NairobiNchini Kenya, ni mbio dhidi ya wakati kutafuta manusura wanaowezekana baada ya jengo lililokuwa likijengwa kuanguka siku ya Ijumaa, Oktoba 23, katika wilaya ya Eastleigh mashariki mwa Nairobi, mji mkuu. Watu wengine wawili waliokolewa kutoka kwenye vifusi siku ya Jumamosi, kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya.
rfi.myMashindano ya mbio za magari, Dakar ya 2027, hayatafanyika Saudi Arabia, kulingana na waandaajiMashirika ya mbio za magari ya Amaury Sport Organisation (A.S.O.) yamethibitisha kuwa mbio za Dakar 2027 hazitafanyika nchini Saudi Arabia, kutokana na mazingira ya kiusalama na matukio yanayoendelea katika kanda hiyo.
rfi.myDRC: Wajumbe wa Upinzani wa Jukwaa la C64 kukutana RomaViongozi wa upinzani kutoka muungano wa Coalition Article 64 (C64) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wanatarajia kukutana Rome, Italia, tarehe 26 Oktoba 2026, kama sehemu ya ziara yao ya kisiasa barani Ulaya. Viongozi watano wakuu wa muungano huo wamethibitisha kuwa watahudhuria mkutano huu. Mkutano huo, unaolenga kushughulikia masuala mbalimbali na kufafanua misimamo, ni sehemu ya ziara pana zaidi barani Ulaya.
rfi.myDRC: Felix Tshisekedi amshambulia vikali mtangulizi wake Joseph KabilaRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RDC), Felix Tshisekedi, amefanya mkutano wake wa kwanza rasmi wa kisiasa siku ya Jumamosi, Oktoba 24, 2026, mjini Kinshasa, ambapo alimshambulia vikali mtangulizi wake Joseph Kabila na kuhamasisha wanasiasa wa muungano wake kukabiliana na uasi mpya.
rfi.myKona kali, jua kali na mashabiki: Waendesha baiskeli watathmini kozi ya KisumuKona nyingi, milima yenye changamoto, upepo mkali na jua kali. Hayo ni baadhi ya mambo yanayowakabili waendesha baiskeli katika Mashindano ya Afrika ya Baiskeli za Barabarani yanayoendelea mjini Kisumu, huku baadhi ya washiriki wakisifu ubora wa kozi hiyo na wengine wakisema ilihitaji umakini mkubwa na maandalizi ya kutosha.
rfi.myNieuwoudt na Mellett wa Afrika Kusini watawala mbio za wanawake KisumuMagda Nieuwoudt amevikwa taji la malkia wa mbio za barabarani za wanawake mahiri, huku Marzaan Mellett akitwaa dhahabu katika kitengo cha wanawake wasiozidi umri wa miaka 23, katika siku ya nne ya Mashindano ya Afrika ya Baiskeli za Barabarani yanayoendelea mjini Kisumu.
rfi.myUfaransa: Jean-Luc Mélenchon atoa wito kwa Emmanuel Macron "kukubali" madai ya waandamanajiUfaransa inapitia siku nyingine ya maandamano ya kiraia leo Jumamosi, Oktoba 24, huku maandamano kadhaa yakitarajiwa. Serikali imeimarisha kwa kiasi kikubwa hatua za usalama kufuatia uharibifu na uporaji wa wiki iliyopita, picha zake zikionekana kote ulimwenguni. Vurugu za polisi pia ziliharibu matukio ya Oktoba 17 na kuibua maswali mengi kuhusu udhibiti wa usalama.
rfi.myDRC: Rais wa zamani wa Baraza la Seneti Alexis Thambwe Mwamba aitishwa tena na mamlakaIngawa alikamatwa asubuhi ya Ijumaa, Oktoba 23, huko Kinshasa, Rais wa zamani wa baraza la Seneti Alexis Thambwe Mwamba aliachiliwa jioni hiyo hiyo. Hata hivyo, mshirika huyu wa zamani wa karibu wa Joseph Kabila hakukamatwa na usalama wa taifa kwa uhusiano wake na rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambaye anaongoza uasi wa FRN.